LEO KATIKA HISTORIA: Machi 24


Björn Kuipers


1984: Christopher Samba azaliwa
Mchezaji wa Dynamo Moscow na timu ya taifa ya Congo Christopher Samba alizaliwa mjini Crétil nchini Ufaransa. Aliwahi kucheza Queens Park Rangers (England) akitokea Anzhi ya Urusi. Tangu alipotua jijini Moscow mwaka 2013 ametupia mabao 5 katika mechi 25. Alianza kuichezea Congo Brazzaville akiwa na umri wa miaka 20.

1973: Björn Kuipers azaliwa
Huyu ni mwamuzi wa soka kutoka nchini Uholanzi. Aliingia katika orodha ya waamuzi wa Fifa tangu mwaka 2006. Mwaka 2011 alichezesha UEFA Super Cup. Alizaliwa Oldenzaal. Kuipers amesoma katika Chuo Kikuu cha Radboud, Nijmegen masuala ya Utawala wa Biashara. Katika Kombe la Dunia nchini Brazil (2014) alichezesha mtanange wa kundi E  kati ya Uswisi na Ufaransa pia katika hatua ya 16 Colombia ilipowabanjua Uruguay mabao 2-0. Pia alionekana katika ukurasa wa mbele wa kitabu cha Sheria za Mchezo cha FIFA 2014/15.

2013: Heinz Patzig afariki
Heinz alikuwa mjerumani ambaye alizaliwa Septemba 19, 1929 mjini Chemnitz na kufariki mjini Braunschweig. Alikuwa mchezaji wa soka wa zamani na kocha ambapo mwaka 1950 alikimbilia Ujerumani Magharibi  ambako alipata mafanikio ya juu akiwa na VfB Lübeck pia Eintracht Braunschweig hadi majeruhi yalipomfanya astaafu soka mwaka 1961.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks