Timu ya taifa ya Uingereza imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 Lithuania katika mchezo wa Kundi E wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Ulaya uliofanyika usiku wa jana kwenye Uwanja wa Wembley.
Mabao ya Uingereza yalifungwa na na wachezaji Wayne Rooney katika dakika ya sita hilo likiwa bao lake la 47 kwenye timu ya taifa, Danny Welbeck alifunga bao la pili dakika ya 45,Raheem Sterling alifunga bao la tatu dakika ya 58 huku Harry Kane akihitimisha kalamu ya mabao katika dakika ya 71 ikiwa ni mara yake ya kwanza kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.
Kwa Ushindi huo Uingereza imefikisha pointi 15 baada ya mechi tano na kuendelea kujikita kileleni mwa kundi E, mbele ya Slovenia yenye pointi tisa sawa na Uswisi, wakati Lithuani ina pointi sita.
Kikosi cha Uingereza ; Hart, Clyne, Cahill, Jones, Baines, Henderson/Barkley dk71, Carrick, Delph, Sterling, Welbeck/Walcott dk76 na Rooney/Kane dk71.
Kikosi cha Lithuania; Arlauskis, Freidgeimas, Zaliukas, Kijanskas, Andriuskevicius/Slavickas dk83, Chvedukas, Zulpa, Mikuckis/Stankevicius dk66, Mikoliunas/Kazlauskas dk88, Cernych na Matulevicius.
0 comments:
Post a Comment