LEO KATIKA HISTORIA: Machi 30


Sergio Ramos

1997: Elkington ashinda ubingwa wa Gofu
Mkali huyu wa gofu kutoka nchini Australia ambaye aliwahi kukaa majuma 50 katika ‘Top 10’ ya orodha ya wachezaji bora wa gofu katika kipindi cha mwaka 1995-1998, alizaliwa Inverell, New South Wales Desemba 2, 1962. Sasa ana umri wa miaka 53. Alitwaa taji la Golf’s Players Championship.

1986: Sergio Ramos azaliwa
Huyu ni mwanasoka wa Hispania na klabu ya Real Madrid alizaliwa Camas, Sevilla. Hadi sasa anaongoza kwa kuwa mfungaji bora wa safu ya ulinzi wa La Liga. Kocha wake wa sasa anamfananisha na mkongwe Paolo Maldini. Pia katika mechi dhidi ya Ukraine waliyocheza hivi karibuni alikuwa akisheherekea miaka 10 ya kuitumikia La Roja.

1978: Harold Gimblett ajiua
Gimblett alikuwa mchezaji wa Kriketi katika klabu ya Somerset na England. Alikuwa akijulikana kwa kasi awapo uwanjani. Mwaka 1982 aliandikwa katika kitabu cha David Foot akisifiwa kwa umahiri wake kama ‘batsman’. Alijiua kwa kunywa dozi kubwa ya vidonge Verwood, Dorset. Alizaliwa Bocknoller katika vilima vya Quantock magharibi mwa Somerset Oktoba 19, 1914.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks