Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa
ya Ufaransa Zinedine Zidane amesema kuwa ana matarajio ya kuiongoza timu ya
taifa ya Ufaransa kwa siku za mbeleni.
Hata hivyo Zidane ameongeza kuwa endapo hatakuwa kocha mkuu wa
timu hiyo basi ataangalia mambo mengine ambayo anaweza kufanya ndani ya kikosi
hicho.
Wakati Zidane anaongea na chombo cha habari cha Canal+Francia
alisema kuwa” nadhani mmenielewa, malengo na matarajio yangu nikuwa kocha wa
timu ya Ufaransa lakini sijuhi ni lini na siku gani maana bado nina muda wa
kusonga mbele”.alisema Zinedine.
Nyota huyo enzi za uchezaji wake aliweza kunyakuwa makombe
mbalimbali kama,kombe la dunia, kombe la mabingwa ulaya pamoja na medali nyingi
na kwasasa ni kocha wa kikosi cha akiba cha wachezaji wa klabu ya Real
Madrid.

0 comments:
Post a Comment