Rais Kikwete awaonya viongozi wa dini
Rais Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kuacha kuwasilikiza wanasiasa pamoja na viongozi wa dini wanaowashawishi kuipigia kura ya hapana katiba iliyopendekezwa, Rais amesema kuwa katiba hii ni bora kuliko inayotumika kwasasa.
Pia amewaonya Viongozi wa Dini kuacha kuhamasisha waumini wao kuipigia Kura ya Hapana Katiba maana kwa kufanya hivyo wanaingilia Uhuru binafsi wa mtu kuamua mambo yake.
Rais Kikwete alieleza hayo katika Mkutano wake na Viongozi wa Dini wanaounda Kamati ya Amani kwa Mkoa wa Dar es salaam ambapo mikoa mbalimbali iliwakilishwa na baadhi ya viongozi.

0 comments:
Post a Comment