Wachezaji 15 watolewa nje kwa kadi nyekundu
Jana nchini Uturuki limetokea tukio la kushangaza kwenye ulimwengu wa soka baada ya mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo kumalizika kwa wachezaji jumla wa 15 wa timu mbili pinzani kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Tukio hilo lilitokea wakati mchezo unakaribia kumalizika, wachezaji wa timu hizo walianza kubishana na wengine wakipigana baada ya kutokea faulu.
Baada ya mzozo huo kutulia mwamuzi wa mchezo huo aliwatoa nje kwa kadi nyekundu wachezaji 15 ambao walikuwa wanapigana na kubishana huku timu moja wakitolewa wachezaji 7 na timu nyingine wachezaji 8.
Na mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya bao1-0.

0 comments:
Post a Comment