
Alyn Camara
|
1931: Knute Rockne afariki
Knute Rockne alikuwa mwanasoka wa zamani na kocha katika Chuo Kikuu cha Notre Dame (Marekani). Alizaliwa Machi 4, 1888 Voss nchini Norway. Alifariki dunia kwa ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 43. Chuo cha Notre Dame kimeweka utaratibu wa kumkumbuka mkali huyu.
1989: Alyn Camara azaliwa
Huyu ni mwanariadha wa ‘miruko ya chini’ kutoka nchini Ujerumani akiweka rekodi ya kushiriki michuano ya olimpiki mwaka 2012 licha ya kushindwa kufuzu. Alizaliwa Bergisch Gladbach. Kwa mara ya kwanza alianza kuonekana mwaka 2011 katika michuano ya Ulaya chini ya umri wa miaka 23 iliyofanyika Ostrava, Czech ambako alishika nafasi ya saba akiruka kwa mita 7.71
2013: Dmitri Uchaykin alifariki
Uchaykin alikuwa mchezaji wa ‘Ice Hockey’ kutoka nchini Russia, nafasi ya winga wa kushoto. Alizaliwa Juni 10, 1980 mjini Khabarovsk, USSR. Alifariki katika michuano ya Kazakhstan Hockey alipogongana na Donatas Kumeliauskas na baadaye alipelekwa hospitalini alikofia. Alimuacha mkewe akiwa mjamzito.
0 comments:
Post a Comment