Mlinda mlango wa klabu ya Chelsea Peter Cech amesema kwasas anataka kuondoka kwenye klabu hiyo yenye maskani yake jijini London.
Cech amekuwa mlinda mlango namba moja wa Chelsea kwa miaka kumi, msimu huu amekuwa akikosa kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Jose Mourinho baada ya mlinda mlango Thibaut Courtois kurudi kutoka Atletico Madrid ambapo alikuwa amepelekwa kwa mkopo.
Ndani ya msimu huu Peter Cech amecheza michezo 14 mpaka sasa.
Wakati Peter alipokuwa anahojiwa na mwandishi wa gazeti la Idnes alisema” sijuhi klabu inafikiria nini labda inaangalia ni nani anafanya vizuri kati wangu na Thibaut lakini nitakuwepo msimu huu tu maana sitaki kuendelea kukaa hivi” Alisema Cech.
Cech alijiunga na Chelsea mwaka 2004 na amefanikiwa kubeba makombe matatu ya ligi ya mabingwa, makombe manne ya FA na makombe matatu ya ligi kuu mchezo wake wa mwisho kucheza msimu huu ulikuwa ni mchezo wa Chelsea na Tottenham timu hiyo iliibuka na ushindi wa magoli 2-0.

0 comments:
Post a Comment