Ronaldo huwenda akapewa adhabu kali


Ronaldo akishangilia goli
Ronaldo akishangilia goli
Nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo anaweza kukumbwa na adhabu kutokana na ushangiliaji wake aliouonesha siku ya jumapili alipofunga goli dhidi ya mahasimu wao wa jadi Barcelona.
Siyo mara ya kwanza Ronaldo kufunga goli kwenye uwanja wa Nou Camp lakini siku ya jumapili baada ya kufunga alionesha kitendo ambacho mashabiki wa Barcelona wamedai kuwa alikuwa alikuwa anawatukana.
Mashabiki wamesema siyo mara ya kwanza kwa nahodha huyo wa Ureno kuonesha kitendo hicho bali imekuwa kawaida yake ya kuwatukana mashabiki wa upande wa upinzani wakati anapofunga goli, kitendo kama hicho kilitokea kwenye mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita dhidi ya Atletico mchezaji huyo alivua shati na kuwarushia mashabiki wa upande wa pili.
Rais wa ligi ya Hispania  amesema  huwa wanakuwa makini kufatilia ishara ambazo uoneshwa na wachezaji wanapofunga magoli au pindi mchezo unapokuwa unaendelea kwahiyo bado wanafatilia na kama itagundulika kuwa alifanya kosa hilo basi mchezaji huyo atawajibishwa.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks