Mwanamke Debra Milke aliyekuwa ameshtakiwa kwa kosa la kumuua mwanawe wa miaka minne mwaka wa 1990 hatimaye ameachiwa huru baada kutumikia kifungo cha miaka 25.
Tuhuma dhidi ya Debra zilidai kuwa mwanamke huyo alimuua mwanawe Christopher ili aweze kupata fidia kutoka kwa shirika la bima la Marekani.
Debra mwaka 1990 aliachiliwa kwa dhamana ya dola 250,000, mwaka wa 1991 mwanamke huyo alikamatwa tena baada ya mwili wa mwanawe kupatikana.
Baada ya kuzuiliwa kwa miaka 25 hakimu katika mahakama moja jimboni Arizona ameamua kumwachia huru Debra kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha juu ya kesi hiyo
 
 

0 comments:
Post a Comment