Sasa yamekuwa licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Hii inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
Hata hivyo, kwa mujibu wa viongozi waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari Jumapili ya Machi 22.
Endelea kufuatilia nellychazzy kwa tukio hilo tutakalowaletea kila kitakachojiri katika mkutano huo, kujua ni wapi na muda gani endelea kuperuzi nasi.
ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.



0 comments:
Post a Comment