LEO KATIKA HISTORIA: April 1


1392: Siku ya Wajinga yatambuliwa
Clarence Seedorf
Aprili Mosi hutambuliwa kuwa ni siku ya wajinga duniani, watafiti wa masuala mbalimbali waligundua kuwa ipo katika matukio yalikusanywa na  Geoffrey Chaucer wa Cantebury mwaka 1392. Matukio hayo yalihusu kipindi cha miaka 100 ya vita. Siku hii imejawa na utani  na vituko ambavyo vinahusu maisha ya kila siku ya watu. Baadhi ya vyombo vya habari huweza kutoa taarifa za utani usipoziangalia vizuri hutagundua kuhusika na siku hii. Siku hii ilipanda nguvu sana karne ya 19 mpaka sasa nchini Marekani, Canada, Australia na Brazil.

1976: Seedorf azaliwa
Huyu ni mwanasoka wa zamani wa Uholanzi na klabu ya AC Milan, alizaliwa Paramaribo nchini Suriname lililokuwa koloni la Wadachi. Alianza soka lake katika klabu ya Ajax. Clarence Seedorf ametwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na vilabu vya Ajax (1995), Real Madrid (1998) na AC Milan (2003, 2007). Anaongea lugha sita ambazo ni Kidachi, Kiingereza, Kiitaliano, Kihispaniola na Kisuriname. Ana watoto wanne. 

2013: Karen Muir afariki dunia
Karen Muir alikuwa mtaalamu wa kuogelea na daktari kutoka nchini Afrika Kusini. Alizaliwa Septemba 16, 1952 mjini Kimberley akisoma katika shule ya Diamantveld. Alifariki dunia kwa kansa ya matiti akiwa na umri wa miaka 60 mjini Mossel Bay, Magharibi mwa Port Elizabeth. Agosti 10, 1965 akiwa na umri wa miaka 12 miezi 10 na siku 25 aliweka rekodi ya kutwaa taji la kuogelea katika ‘ASA National Junior Championship’ nchini England akiogelea yadi 110 kwa dakika 1:08.7
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks