LEO KATIKA HISTORIA: April 2

Teddy Sheringham

1939: Marvin Gaye azaliwa
Huyu alikuwa ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo  kutoka nchini Marekani akijipatia umaarufu mkubwa miaka ya 1960 hadi 1970 akiwa na Motown Records. Kibao cha “Sexual Healing” na Midnight vilimpa umaarufu hadi kutwaa Tuzo ya Grammy mwaka 1982. Aliuawa na baba yake Aprili 1, 1984 nje ya nyumba yao wilayani West Adams, Los Angeles. Alizaliwa jijini Washington  wakiishi katika mtaa wa kwanza wa 1617 SW  baadaye walihamia Deanwood kaskazini Mashariki mwa Washington.

1966: Sheringham azaliwa
Jina lake halisi ni Edward Paul Sheringham akifahamika zaidi kama Teddy Sheringham kutokana na uwezo mkubwa kufumania nyavu. Kwa sasa anafanya kazi na klabu ya West Ham United akiwanoa wachezaji katika safu ya ushambuliaji. Mwingereza huyu  alicheza soka miaka 24 akianzia Millwall (1983-1991) baadaye Nottingham Forest. Amewahi kuzitumikia Tottenham, Manchester United na Portsmouth. Alistaafu soka akiwa na umri wa miaka 42 akiitumikia Colchester United.

1995: Aboud Nef azaliwa
Huyu ni mwanasoka chipukizi alipoteza maisha akiwa na umri wa miaka 18 mjini Boumerdès nchini Algeria katika ajali mjini humo Novemba 5, 2013. Abdelouahab Nave alizaliwa Boumerdès akicheza safu ya kiungo katika Akademi  ya El-Ankaoui Jean-Marc Guillou. Alipoteza maisha wakati akienda mazoezi katika viwanja vya JMG-PAC Talasa El Merdja. Aliwahi kufanya majaribio FC Porto (Ureno) na Lyon (Ufaransa).
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks