Raheem Sterling ameiamba BBC Sport kuwa si “kijana (20) mpenda-fedha” baada ya kuthibitisha kukataa mkataba wa pauni 100,000 kwa wiki Liverpool.
Pia anasema hatajadili mkataba mpya na Reds mpaka msimu wa jua, bila kujali mkataba ni mkubwa kiasi gani ambao atapewa kwa wakati huo.
“Sio kuhusu pesa kabisa,” alisema mshambuliaji wa Uingereza.
“Haijawahi kuhusu fedha. Nazungumzia kushinda mataji kwenye maisha yangu. Hich ndicho ninachozungumzia.”
Aliongeza: “Sizungumzii ni magari mangapi nitakwenda kuendesha, nyumba ngapi nilizonazo. Nataka kuwa bora nitakavyoweza kuwa.”
Sterling alijiunga Reds kutoka QPR mwaka 2010, hakuwa mchezaji wa timu ya kwanza mpaka msimu uliofuata.
“Sitaki nieleweka kama kijana mpenda fedha,” alisema mchezaji huyo, ambaye amebakisha miaka miwili katika mkataba wake wenye thamani ya pauni 35,000 kwa juma.




0 comments:
Post a Comment