![]() |
Lucas Radebe na Nelson Mandela
|
1941: Bobby Moore azaliwa
BOBBY Moore alikuwa mahiri katika kusakata kabumbu akiwa na klabu ya West Ham United akicheza mechi 544 na kutupia mabao 24. Jina lake halisi ni Robert Fredrick Chelsea, alizaliwa katika kitongoji cha Barking, kilichopo katika jimbo la Essex, Mashariki mwa London. Alifariki akiwa na umri wa miaka 51, Februari 24, 1993.
1948: Marcelo Lippi azaliwa
ANAKUMBUKWA kwani mwaka mwaka 2006 akiwa kocha wa Azzuri alitwaa Kombe la Dunia nchini Ujerumani. Alichukua nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya Italia mwaka 2008 akipokea mikoba ya Cesari Prandelli. Alizaliwa Viareggio, mji uliopo katika pwani ya bahari ya Tyrrhenian, kaskazini mwa Tuscany, Italia.
1969: Lucas Radebe azaliwa
HAYATI Nelson Mandela aliwahi kukaririwa akisema “Radebe is my hero” yaani Radebe ni shujaa wangu. Mkali huyu alianza kucheza soka katika klabu ya Kaizer Chiefs na baadaye Leeds ya Uingereza ambako alicheza mechi 200 akipewa majukumu ya unahodha yaliyomfanya ajulikane hata kupewa jina la “The Rhoo” yaani Chifu. Lucas Valeriu Ntuba Radebe alizaliwa Soweto, Afrika Kusini sasa ana miaka 46.
0 comments:
Post a Comment