LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 26

Waamuzi wakijadiliana jambo NBA

1564: Shakespeare azaliwa
WILLIAM Shakespeare alikuwa mtunzi wa mashairi na mwigizaji raia wa Uingereza ambaye anachukuliwa kama ndiye mwandishi mkubwa wa lugha ya kiingereza. Alizaliwa Stratford-upon-Avon. Alipofikisha miaka 18 alimuoa Anne Hathaway ambaye walizaa watoto watatu, Susana  na mapacha Hamnnet na Judith. Kati ya mwaka 1585-1592 alikuwa maarufu kwa uigizaji jijini London. Alifariki Aprili 23, 1616.
1988: Waamuzi watatu waanza kutumika NBA
CHAMA cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani  (NBA) kilipitisha matumizi ya waamuzi  watatu katika mechi mbalimbali za Ligi Kuu nchini  humo. Kanuni hiyo ilianza kutumika kwa mara ya kwanza msimu wa 1988-89 tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo Juni 6, 1946 jijini New York.
2014: Lee Marshall afariki dunia
MARSHALL Aaron Mayer alikuwa mtangazaji wa mieleka nchini Marekani chini ya Mwavuli wa Chama cha Mieleka nchini humo (AWA), pia World Championship Wrestling (WCW) na Women Wrestling (WOW).
Alizaliwa Novemba 28, 1949 Los Angeles alikuwa akijulikana kwa jina ‘Stagger Lee’ akijiunga na timu ya watangazaji wa mchezo huo wakati wa mapambano mbalimbali katika runinga ya ESPN.
Atakumbukwa kwa sauti yake iliyokuwa na mvuto yenye kuamsha shangwe ukumbini wakati wa mchezo huo akiwapandisha jukwaani wakali mbalimbali. Alifariki Santa Monica, California.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks