LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 6

Babatunde Olatunji
1985: Ongfiang azaliwa
Frank Ongfiang ni mchezaji wa kabumbu kutoka nchini Cameroon ambaye anaitumikia klabu ya Zirka Kirovohrad (Ukraine).
Alizaliwa mjini Yaounde akianza soka katika klabu ya Bordeaux nchini Ufaransa. Msimu wa 2001-02 alisajiliwa na klabu ya Venezia nchini Italia. Alicheza mechi yake ya kwanza Serie A Machi 17, 2002 dhidi ya Chievo. Kwa wakati huo alikuwa mchezaji wa nne wa kigeni mwenye umri mdogo kucheza ligi kuu nchini humo.

2003: Babatunde afariki dunia
Babatunde Olatunji alikuwa mpiga ngoma, mwalimu na mwanaharakati wa Nigeria alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 75. Olatunji alizaliwa Aprili 7, 1927 katika kijiji cha Ajido karibu na mji mdogo wa Badagry katika jimbo la Lagos, Kusini Magharibi mwa Nigeria. Alipata ufadhili wa Rotary ambao ulimpeleka kusoma nchini Marekani katika Chuo cha Morehouse kilichopo Atlanta katika jimbo la Georgia. Alirekodi nyimbo zake chini ya nembo ya Columbia.

2013: Norgrove alifariki dunia
Michael Norgrove alikuwa bondia mzaliwa wa Zambia aliyekuwa akiishi nchini England. Akiwa London alikuwa akijulikana kwa jina la Zambesi Hitman. Hadi kufa kwake aliweka rekodi ya kutopoteza pambano hata moja. Kabla mauti hayajamkuta alianza kuumwa hali iliyofanya apelekwa hospitalini ambako alipoteza maisha. Kuanzia hapo mjadala mkubwa uliibuliwa kuhusu usalama wa mabondia na mchezo kwa ujumla, kwani haikujulikana nini kilimuua mkali huyo. Alizaliwa Januari 9, 1981 mjini Kabwe kwa baba Mwingereza aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Reli la Zambia ambaye alipomaliza mkataba wake Michael alikuwa na umri wa miaka saba wakahamia Australia na baadaye Manchester nchini Uingereza.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks