![]() |
Steven Charles Kanumba
|
1983: Ribéry azaliwa
Frank Henry Pierre Ribéry ni mchezaji wa kabumbu kutoka nchini Ufaransa, ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Pia mkali huyu hujulikana kwa jina la Bilal Yusuf Mohammed baada ya kujiunga katika dini ya Uislam mwaka 2006. Alizaliwa Boulogne-sur-Mer, Kaskazini mwa Ufaransa.
Alianza kucheza soka lake mwaka 1989 katika klabu ya Conti Boulogne, miaka saba baadaye alitua Lille LOSC. Katika timu ya taifa amecheza mechi 81. Mwaka 2013 alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya.
Mkali wa zamani wa soka Zinedine Zidane hupenda kumwita “Kito cha thamani cha Ufaransa”
2012: Kanumba afariki dunia
Steven Charles Kanumba alikuwa mwigizaji na muongozaji wa filamu nchini Tanzania. Alizaliwa Januari 8, 1984 katika ardhi ya Usukuma mkoani Shinyanga na kufariki dunia Aprili 7, 2012 jijini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 28. Pia Kanumba alionekana katika filamu za Nollywood.
Mpenzi wa Kanumba wakati huo Elizabeth "Lulu" Michael Kimemeta ndiye chanzo kikubwa cha mauti ya nyota huyo maarufu nchini Tanzania.
Kanumba alizikwa katika makaburi ya Kinondoni inakadiriwa watu zaidi ya 20,000 walihudhuria, wakiwemo Mke wa Rais Jakaya Kikwete, mama Salma na Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal.
2014: Waltman afariki dunia
Royce Waltman alikuwa mchezaji wa zamani na Kocha wa mpira wa kikapu katika Chuo Kikuu cha Indiana State, Indianapolis na DePauw nchini Marekani.
Akiwa kocha alishinda michezo zaidi ya 100 katika michuano ya mpira wa kikapu kwa wanavyuo (NCAA) nchini humo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 kutokana na afya yake kuwa mbaya. Alizaliwa Januari 8, 1942.
0 comments:
Post a Comment