Mwezi huu nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona ataungana na nyota wengine ambao hawajatajwa kwa majina kucheza mchezo wa kuiunga mkono nchi ya Colombia katika hatua yake ya kuelekea kwenye kipindi cha amani.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa jijini Bogota nchini humo.
Maradona anakumbwa kwenye fainali za dunia za mwaka 1986 alipofunga bao la mkono na kuliita ( Hand of God) yaani mkono wa Mungu.
Mchezo huo unaonekana utatoa mitisha kwa serikali ya Colombia kuendelea na mazungumzo na kikundi cha waasi cha FARC ili kuangalia uwezekano wa kumaliza umwagaji damu unaoendelea nchini humo.
Inasemekana kuwa mgogoro wa mwaka 1964 nchini humo ulipoteza maisha ya watu milioni 22
0 comments:
Post a Comment