1968: Ufunguzi Baseball waahirishwa
UFUNGUZI wa Mashindano ya Baseball nchini Marekani uliahirishwa kwasababu ya mauaji ya Martin Luther King Jr. ambaye alikuwa mwanaharakati wa Wamarekani weusi. Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel aliuawa Loraine Motel, Memphis, Tennessee Alhamisi ya Aprili 4, 1968. Muuaji James Earl Ray alikamatwa Juni 8, 1968 jijini London na kuhukumiwa miaka 99.
1986: Akinfeev azaliwa
MLINDA mlango wa timu ya taifa ya Russia, Igor Akinfeev ambaye hivi karibuni alitupiwa kipande cha moto katika mtanange wa kufuzu kucheza UEFA Euro 2016 alizaliwa Vidnoye jijini Moscow. Kwa sasa anaitumikia klabu ya CSKA Moscow.
2014: The Ultimate Warrior afariki dunia
JINA lake halisi ni James Brian Hellwig mwanamieleka maarufu kutoka nchini Marekani. Alikuwa katika WWE tangu mwaka 1987 hadi kustaafu kwake mwaka 1998. Alifariki akiwa na umri wa miaka 54, Scottdale katika jimbo la Arizona akiwa na familia yake. Enzi za uhai wake aliweka rekodi ya kumcharaza mkali Hulk Hogan katika pambano la WrestleMania VI.
0 comments:
Post a Comment