Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameponda kiwango cha wachezaji wa Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ katika mchezo walionyukwa mabao 8-0 na Yanga.
Kocha huyo alisema kutokana na Coastal kucheza chini ya kiwango Yanga ingekuwa makini ingeshinda mabao 10.
Akizungumza Dar es Salaam, kocha huyo machachari alisema ingekuwa Simba ingepata ushindi mnono wa zaidi ya mabao manane iliyopata Yanga.
Julio aliyewahi kuichezea Simba miaka ya nyuma alisema Yanga ilicheza soka ya kawaida sana.
“Yanga walicheza kiwango cha kawaida, ingekuwa Simba tungefungwa zaidi ya 10,” alisema Julio.
0 comments:
Post a Comment