LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 9


Robbie Fowler


1925: Bambino afikishwa hospitali
Jina lake halisi ni George Herman “Babe” Ruth. Huyu ni mkali wa mchezo wa baseball wa nchini Marekani aliyecheza misimu  22 ya ligi kuu ya baseball nchini humo (MLB). 

Mashabiki walimpa jina la ‘The Bambino’ pia ‘The Sultan of Swat’ akitumia mkono wa kushoto na klabu ya Boston Red Sox. Alizaliwa Februari 6, 1895 na kufariki Agosti 16, 1948.

1969: Linda Kisabaka azaliwa
Linda Kisabaka ni mwanariadha wa zamani kutoka nchini Ujerumani katika mbio za mita 400 na 800. Alistaafu kukimbia mwaka 2001. 

Alizaliwa Wuppertal, mashariki mwa mji wa Dusserdorf, katika jimbo la North Rhine-Westphalia. Alizitumikia klabu za Bayer 04 Leverkusen na LAZ Leipzig. Muda mzuri aliowahi kukimbia ni dakika 1:58.24 alioupata Agosti 1996 jijini Zurich.

1975: Robbie Fowler azaliwa
Robert Bernard “Robbie” Fowler ni mchezaji wa soka wa zamani na kocha mzaliwa wa Uingereza ambaye aliitumikia kwa mafanikio klabu ya Liverpool. 

Alizaliwa Toxteth, ndani ya jimbo la Lancashire ambako Liverpool inapatikana. Aliweka rekodi ya kufunga mabao 183 akiwa na Liverpool. Aliwahi kuzitumikia Leeds na Manchester City. 

Anakumbukwa kwa tukio la Machi 24, 1997 alipomuomba mwamuzi kutoamuru penati ipigwe licha ya yeye kuangushwa na mlinda mlango wa Arsenal wakati huo David Seaman.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks