Kikosi cha Madrid kikiwa nyumbani kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 9-1 dhidi ya Granada katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania La Liga.
Ushindi wa Madrid umepatika kupita kwa wachezaji Cristiano Ronaldo mabao matano katika dakika ya ( 30, 36, 38, 54, 91 ), Karim Benzema mabao mawili katika dakika ya ( 52, 56 ) na bao moja kupitia kwa Gareth Bale katika dakika ya 25.
Kwa ushindi huo Madrid imerudi kwenye mbio za kupigania ubingwa wa ligi kuu ya La liga huku ikitoa salamu kwa washindani wake kuwa wao hawajakata tamaa ya kupigania ubingwa huo.
Upande wa rekodi unaonesha kuwa mara ya mwisho Granada kuifunga Madrid ilikuwa ni mwaka 1974 ambapo iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kikosi cha Madrid ni: Casillas, Arbeloa, Varane, Ramos, Marcelo, Modric, Kroos, James, Bale, Benzema, Ronaldo
Benchi : Navas, Coentrao, Nacho, Illarramendi, Lucas Silva, Jese, Chicharito.
Kikosi cha Granada: Oier; Foulquier, Babin, Mainz, Juan Carlos; Fran Rico, Iturra; Ibanez, Rochina, Candeias; El-Arabi.
Benchi : Nyom, Javi Marquez, Piti, Riki, Roberto, Eddy, Murillo.
0 comments:
Post a Comment