
Steve Beaton ni mchezaji wa vishale(darts) kutoka England ambaye aliweka rekodi ya kutwaa taji la BDO mwaka 1996. Alizaliwa Coventry, Warwickshire nchini humo. Alishiriki mashindano ya dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1992 akipoteza katika mzunguko wa kwanza dhidi ya Chris Johns lakini mwaka uliofuata alifanya vizuri akimshusha bingwa mtetezi Dennis Priestley.
1981:Stefan Ludik azaliwa
Stefan Ludik ni mchezaji wa kriketi, msanii wa filamu na mwimbaji kutoka nchini Namibia. Ameshiriki programu ya Big Brother Africa na kuwa mwakilishi wa kwanza kutoka Namibia. Aliitumikia timu ya taifa chini ya umri wa miaka 19 mwaka 2000, akicheza katika nafasi ya batsman wa kulia na ‘medium pace bowler’. Alizaliwa jijini Windhoek.
1982: Kelly Pavlik azaliwa
Kelly Robert Pavlik ni bondia aliyestaafu kutoka nchini Marekani. Alitwaa taji la The Ring, WBC, na WBO middleweight baada ya kumdunda Jermain Taylor Septemba 29, 2007. Mataji hayo aliyapoteza Aprili 17, 2010 baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa Sergio Martinez. Alizaliwa kusini mwa Jimbo la Ohio, Youngstown. Amecheza mapambano 42 akishinda 40 akipoteza mawili .
0 comments:
Post a Comment