Blatter aipongeza Yanga


Rais wa Fifa Sepp Blatter
Rais wa Fifa Sepp Blatter
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani – FIFA, Joseph Blatter ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi kufuatia klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Katika salamu hizo za Blatter, amemuomba Rais wa TFF kufikisha salamu zake za pongezi kwa klabu ya Young Africans, wanachama, wapenzi wa mpira wa miguu kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mwakani katika michuano ya kimataifa barani Afrika.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa 4-0 dhidi ya Polisi Morogoro jana
Wachezaji wa Yanga wakishangilia ubiwa wa VPL 2014/2015 baada ya kuifunga Polisi Moro 4-0
Blatter amesema anatambua mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa, yametokana na na jitihada za uongozi, wachezaji, bechi la ufundi, madaktari, wanachama , washabiki na kila mmoja aliyeshiriki katika kufanikisha kutwaa Ubingwa huo.
Mpira wa miguu unapata mafanikio makubwa kwa kuvuka mipaka hadi kuwa kichochezi halisi cha maendeleo, unawasaidia wachezaji wa ngazi zote kuinua vipaji vyao na mbinu katika kuelekezwa na kubadilika wakati huo huo wakiwa wakiwa na nyoyo za ushirikiano.
Rais wa shirikisho la mpira TFF, Jamali Malinzi
Rais wa shirikisho la mpira TFF, Jamali Malinzi
Aidha Blatter amesema mpira wa miguu kwa sasa ni shule kwa maisha, vijana wa leo wanaweza kufaidika kupitia kucheza mpira wa miguu kwa ngazi ya kijamii na mtu mwneyewe binafsi, ndio maana amewapa salamu za pongezi Young Africans  na kuendeleza kazi yao na kuongoza njia ya mafanikio.
Kujituma kwa klabu ya Young Africans kumewasaidia kushinda Ubingwa huu ikiwa ni ni mara ya 25, huu ni ushindi mkubwa katika mpira wa miguu.

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks