Hukumu ya rais Morsi yapingwa vikali

Said Boumedouha
Said Boumedouha
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelaani vikali hukumu ya kifo dhidi ya rais wa zamani wa Misri Mohammad Morsi na kusema kuwa kesi hiyo haikuzingatia taratibu za mahakama.
Naibu Mkuu wa Amnesty International katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika Said Boumedouha amesema, ‘kwa kuzingatia kuwa Morsi alishikiliwa kwa miezi kadhaa bila kuwepo usimamizi wa mahakama na pia ukweli kuwa hakuwa na wakili wakati wa kesi yake ni mambo ambayo yanapelekea kesi dhidi yake kuwa batili na isiyo na haki.’
Said amesema hukumu hiyo ya kifo ni ishara ya wazi ya kukiukwa haki za binadamu.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks