Marais wa ICTR wampongeza Rais Kikwete


Rais Kikwete akihutubutia Umoja wa Mataifa

Wakati majukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ( ICTR) yakifikia ukingoni mwishoni mwa mwaka huu, hatima ya wafungwa waliomaliza vifungo vyao na wale walioachiwa huru bado haijajulikana.

Wakiwasilisha kwa nyakati tofauti mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, Taarifa ya (ICTR) na Taarifa ya Taasisi ya Kimataifa itakayo hifadhi nyaraka na kumbukumbu zote zinazohusiana  na  mahakama  hiyo (IRM) Marais wa vyombo hivyo, Jaji Vagn Joesen na Jaji Theodor Meron wamesema,  mahali pa kuwapeleka waliomaliza vifungo na walioachiwa bado ni changamoto kubwa.

Marais hao ambao mmoja (Jaji Joesen) alikuwa akiwasilisha taarifa yake ya mwisho kwa upande wa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbali ya  Rwanda, wamepongeza Mhe Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Watanzania kwa kuwa mwenyeji wa ICTR kwa miongo miwili ya  uhai wake.

Akasema Jaji Theodor Meron “Julai mwaka huu, tuliweka jiwe la msingi la makazi mapya yakayoiridhi ICTR,  uwepo wa Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwenye  hafla hiyo ni udhihirisho wa namna gani Tanzania imekuwa ikishirikiana na ICTR  katika utekelezaji wa majukumu yake kuanzia ilipoanza, inapoishia na inakoelekea katika majukumu hake mapya.”

Akaongeza kuwa ujenzi wa makazi hayo mapya  na ambayo yanajengwa katika eneo la  Laki Laki katika jijini la Arusha, unaendelea vema na kwamba nyaraka na kumbukumbu zote  muhimu za ICTR zitakuwa  na mahali salama pa kuzihifadhi na  vikiwamo pia   vyumba  vya mahakama kwaajili ya kumaliza kesi za masalia.

Akasema Taasisi hiyo ya Kimataifa inayochukua nafasi ya ICTR imejianda vema katika kutekeleza  majukumu yaliyombele yake na makabidhiano yanaendelea vema.

Akizungumzia kuhusu  mahali pa kwenda wafungwa waliomaliza vifungo vyao na ambazo mahakama iliwaachia,  Jaji Meron ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kutoa ushirikiano  katika kusaidia   upatikanaji wa makazi mapya kwa watu hao.

Akasema wafungwa waliomaliza vifungo vyao na kuachiwa wanaogopa kurudi  kwenye nchi yao kwa kuhofia usalama wa maisha yao.

Ombi jingine ambalo Jaji Meroe amelitoa mbele  ya Umoja wa Mataifa ni pamoja na  lile la kukamatwa kwa watuhumia ambao wapo mafichoni ili waweze kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Viongozi hao wamesema wao binfasi wamejifunza mengi kutokana na ushiriki wao katika utekelezaji wa kusimamia haki  huku wakisisitiza kuwa katika uhai wake ICTR siyo tu imekuwa chombo cha kutoa haki lakini pia chombo ambacho watu kutoka mataifa mbalimbali na kada tofauti wakiwamo wanafunzi wa  Vyuo Vikuu wamekutumia chombo hicho kama  mahali pa kujifunza, kujielimisha na kujibaharisha.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika  Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, pamoja na kuwashukuru  Marais  hao  kwa utekelezaji wa majukumu yao na kusimamia uanzishwaji wa Taasisi zitakazoridhi kazi za  mahakama ya  ICTR na ICTY naye amesisiza haja na umuhimu wa jumuiya ya kimataifa wa kuwachukua wafungwa waliomaliza vifungo vyao.

Vile vile Balozi Tuvako Manongi amesema wakati Tanzania ikiendelea na kujianda  kuwa mwenyeji wa  IRM,  ingependa kuona kwamba gharama ambazo  si  za lazima za uendeshaji wa  matawi  mawili yanayochukua nafasi ya ICTR ambalo liko Tanzania na ICTY ambalo liko The Hague linazingatiwa.

Chanzo: CCM Blog

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. Casino Games: 5 Best Casinos in Canada
    Best Canadian casino games: Gambling sites, casinos, In Canada, players are allowed 전주 출장안마 to play on 속초 출장안마 mobile devices, 목포 출장안마 or 경상북도 출장마사지 using a 안산 출장안마 mobile device

    ReplyDelete

Blogger Tricks