Moja kati ya madhambi yaliyokuwa yakifanywa na wachezaji wa Dynamo Kiev dhidi ya wachezaji wa Chelsea
Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, amejiweka tena matatani kwa
kumtolea lugha ya kashfa muamuzi, Damir Skomina, aliyechezesha mechi
yao ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi Dynamo Kiev ambapo mechi
iliishia kwa sare ya bila kufungana.
Fabregas (kulia) akiongea na muamuzi, Damir Skomina, (kushoto) akihoji ni kwanini amenyimwa penati ya wazi.
Mourinho alimuita muamuzi huyo kama mtu dhaifu na asiyekuwa na
maamuzi ya busara, baada ya kuinyima timu yake penati ya wazi baada ya
kiungo Cesc Fabregas kufanyiwa madhambi eneo la penati.
Maneno hayo yanaweza kumletea matatizo kocha huyo na ikumbukwe kuwa
ni siku chache tuu zimepita tangu Mourinho atozwe faini ya pauni elfu 50
na chama cha soka nchini Uingereza (FA) kwa kumtolea lugha chafu
mwamuzi, Robert Madeley.
I Run And Own Nellychazy.blogspot.com.
Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting.
Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
0 comments:
Post a Comment