Mume wa zamani wa Irene Uwoya Ndikumana amefariki

Asubuhi ya leo Tanzania imezipokea taarifa za kifo cha aliyekuwa Kocha msaidizi wa timu ya Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana Katauti ambae amefariki ghafla.
Mwandishi wa habari za Michezo shaffi dauda ameripoti kwamba Gakwaya Olivier ambae ni Afisa Habari wa Timu hiyo amesema Ndikumana amefariki kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.
“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli, bado tunasubiri uchunguzi wa kina wa kitabibu”
Marehemu aliwahi kucheza soka Tanzania akiwa na Stand United na ni Mume wa zamani wa  Mwigizaji Irene Uwoya na wana mtoto mmoja
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks