Ashley Young ashtakiwa kwa udhofu wa nidhamu

Ashley Young has made 17 Premier League appearances for Manchester United this season
 Mchezaji wa Manchester United Ashley Young ameshtakiwa kwa udhofu wa nidhamu na shirikisho la kandanda la FA.
Young, 32, alionekana kumgonga kwa mkono mshambuliaji wa Southampton, Dusan Tadic wakati wa mechi iliyotoka sare ya sufuri siku ya Jumamosi.
Refa Craig Pawson hakukiona kisa hicho na Young alistahili kujibu mashtaka hayo hadi leo Jumapili.
Young ambaye alijiunga na Manchseter United mwezi Juni mwaka 2011, alirudi katika kikosi cha England mwezi uliopita baada ya kutokuwepo kwa miaka minne unusu.
United wameshuka hadi nafasi ya tatu katika ligi ya Primia baada ya sare mara tatu mfululizo na kushindwa na Bristol City katika kombe la EFL. kombe la EFL.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks