Unajua mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amezungumza nini na Rais Obama.






Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa amezungumza na Rais Barack Obama kumwelezea kero lake kuhusu udukuzi unaofanywa na serikali kwa mitambo ya Dijital.

Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya ripoti kuwa shirika la ujasusi la Marekani ilibuni mtandao bandia wa Facebook ili kuweza kuvamia mitambo ya Kompyuta inayotumiwa kwa uchunguzi.Zuckerberg mwenye umri wa miaka 29, amesema kuwa serikali ya Marekani inapaswa kupigia debe internet badala ya kuwa adui wa mitandao ya kijamii...>>>>

Shirika la NSA lilisema kuwa taarifa hiyo sio ya kweli.
Mnamo mwezi Septemba, Zuckerberg alisema kuwa Marekani ilikosea sana taarifa zilipoibuka kuwa inafaya udukuzi kwenye mitandao.
Mwanateknolojia huyo alisema kuwa huenda ikachukua muda mrefu sana kwa mageuzi yoyote kufanyika.
Zuckerberg alisema, alisema "wakati wahandisi wetu wanapofanya kila hali kuboresha usalama kwenye mtandao, kwetu ni kama tunawalinda kutokana na wahalifu kwenye mitandao, sio serikali yetu.''
"Serikali ya Marekani lazima ipigie debe Internet sio kuwa adui wa mtandao. Lazima waelezee wanachokifanya la sivyo, watu hawatakuwa na imani tena na serikali.''
Shughuli za shirika la ujasusi la Marekani lilijipata motoni baada ya ufichuzi kutolewa na aliyekuwa jasusi wakati mmoja Edward Snowden, mwaka jana.
Ufichuzi wake ulionyesha kuwa shirika hilo lilikuwa linakusanya taarifa za simu za watu, kufanya udukuzi na kuvamia mitandao ya watu. 

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks