Picha Za Mahabusu alievua nguo Mahakamani Mwanza


Mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji wameleta kizaazaa baada ya kujaribu kutoroka na kukimbilia kwenye mlingoti wa Bendera ya Taifa na kuing’ang’ania kisha kuvua nguo na mmoja wao kubaki mtupu........>>>>>>>>>>
Tukio hilo limetokea May 7 2014 saa nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Nyamagana Mwanza walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao lakini ghafla walipofika kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbio kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa kupaza sauti kudai haki itendeke.
Ni Thobiasi Warioba (35) alieamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu eneo la mlingoti wa bendera ya taifa, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
Watuhumiwa wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro (35), Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine ambaye hakufahamika majina yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 215/2013  na walikamatwa tangu mwaka 2011.

Baada ya kudhibitiwa na askari polisi walisikika wakisema: “haiwezekani tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa, wengine tumebambikiziwa kesi tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie  tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011 tulipokamatwa, tumechoka kukaa mahabusu tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.
Baada ya malalamiko yao askari  mmoja aitwae Inspekta Henry akiwa na wenzake sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie aliwahoji kuhusiana na madai yao huku askari hao wakiwataka kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka Warioba avae nguo ili waweze kuingia Mahakamani.

Mmoja wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza ambae alikataa kutajwa jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao bado haujakamilika na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake zitatajwa tu kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu.






https://soundcloud.com/millard-ayo/mahabusu-mwanza-may-7-2014
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks