Kuhusu Kufungiwa kwa kituo cha TV kilichomuonyesha Rais Museveni kasinzia bungeni.

Screen Shot 2014-06-19 at 3.56.42 PMSerikali ya Uganda imekifungia kituo kikubwa cha Televisheni cha nchi hiyo NTV kuripoti habari zozote zinazomhusu rais baada ya kurusha hewani picha zinazomuonyesha Rais Yoweri Museveni akiwa amesinzia bungeni...>>>>>

Mkurugenzi wa kituo cha habari za serikali Dennis Katungi amenukuliwa akisema kuwa “Rais ana tabia zake wengi mnajua, huwa anatafakari na wanajua lakini bado wameonyesha picha hizo na kusema alikuwa amesinzia.”
Msemaji wa serikali Ofwono Opondo amethibitisha kuwa NTV Uganda itachukuliwa hatua za kinidhamu ambapo wameifungia kuripoti habari zozote zinazomhusu rais wakati bado serikali ikiangalia uhusiano wake na chombo hicho.
Ameituhumu NTV kwa kukosa utaalamu wa uandishi na kuegemea upande mmoja lakini hata hivyo hatua hiyo si ya kudumu ni ya muda tu kuwafanya wafikirie upya.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks