Kuhusu Zitto Kabwe Kuulipia wimbo wa Linex Zaidi ya Milioni 10 na Ujumbe wa Wimbo Huo

Linex na ZittoLinex amepewa sapoti kubwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ili aachie audio na video ya wimbo wake unaoitwa Wema kwa Ubaya...>>>

Linex ameeleza kuwa Zitto Kabwe alimpa idea ya kufanya wimbo ambao angeusapoti lakini Linex akagundua kuwa ana wimbo alifanya mwaka jana na una hisia na ujumbe utakaosaidia kuwapa faraja wengi wenye matatizo, alipomfikishia mheshimiwa aliukubali.
Zitto alivutiwa na ujumbe wa wimbo huo unaohusu watu kutolipiza kisasi na kuendelea kumtegemea Mungu katika kila jambo. Baada ya kuguswa alimfuata Adam Juma na kulipia video hata bila kumwambia Linex, baadae akampa taarifa ajiandae kushuti.
“Tunaanza kushuti next week kwa sababu nilikuwa bado niko busy na Kili Tour. Ni wimbo mzuri utakaoigusa sana jamii halafu baadae tukishashuti tutajua mambo mengine.”
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks