Mchekeshaji mkali Anne Kansiime kutoka Uganda ambaye vichekesho vyake vinaoneshwa katika kituo cha runinga cha Kenya, amechaguliwa kuwa balozi wa kampuni ya Old Mutual....>>>
Kampuni hiyo imemtangaza Kansiime kuwa balozi wao rasmi Jumanne wiki hii na kwamba watamtumia katika kampeni zao katika nchi nzima ya Kenya.
Kansiime anatarajiwa kuwa chachu ya kampeni ya kampuni hiyo inayolenga katika kutoa elimu na kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa bima na mipango ya kifedha.

0 comments:
Post a Comment