TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI HII, KWENYE MAGAZETI YA ULAYA

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI HII
Manchester United imekwisha fahamu wachezaji watano inayowataka, na meneja mpya Louis van Gaal atapewa paundi milioni 220 kuwapata. Van Gaal anataka kumchukua kiungo Kevin Strootman kutoka Roma ya Italia (Daily Express), Frank Lampard ameambiwa hatopewa mkataba mpya na Chelsea, na huenda akaenda kucheza Marekani (Mail on Sunday), Liverpool itasitisha mazungumzo ya mkataba mpya na Raheem Sterling baada ya winga huyo kudai mshahara wa paundi laki moja kwa wiki (Sunday Mirror), beki wa Arsenal, Bacary Sagna amekataa dau kubwa zaidi kutoka Dubai na Monaco, na.......>.>
kukubali mshahara wa laki moja na nusu kwa wiki atakaopewa na mabingwa wa EPL, Manchester City (Sun), Roma wamewaambia Chelsea na Tottenham kuwa watalazimika kutoa si chini ya paundi milioni 50 kama wanamtaka Mehdi Benatia (Metro), Southampton wameweka dau la paundi milioni 30 kwa kila mmoja- Luke Shaw na Adam Lallana. Shaw ananyatiwa na Man United na Liverpool wanamtaka Lallana, na wapo tayari kutoa paundi milioni 25 (Daily Express), Harry Redknapp wa QPR anataka kumsajili beki wa Liverpool Glen Johnson (Daily Star), Everton wanataka kuongeza mshahara wa James McCarthy mara dufu ili asiondoke. Mchezaji huyo kutoka Ireland ananyatiwa na Man United (Daily Star), striker wa Liverpool Luis Suarez atapata ugumu kusema "hapana" iwapo Real Madrid watamtaka, hiyo ni kwa mujibu wa wakili wake (Independent), kipa wa Man U, David de Gea ameitaka klabu yake kumsajili Andres Iniesta kutoka Barcelona (Independent), Barcelona wamesema Cesc Fabregas atapatikana kwa paundi milioni 30. Man United imeacha kumfuatilia, lakini Chelsea, Arsenal na Man City zinamtazama (Daily Telegraph), Man United inaonekana kuzidiwa kete na Barcelona katika kumsajili beki kutoka Ujerumani Marquinhos anayechezea PSG (Daily Express), Man City, Arsenal na Man United zinamfuatilia Xavi wa Barcelona (Daily Star), Arsenal kuanza mazungumzo na Real Madrid kuhusu Karim Benzima na Alvaro Morata (Daily Express), Arsenal pia wanataka kumsajili kipa wa Nice ya Ufaransa, David Ospina (RMC), Liverpool inajiandaa kumsajili kiungo wa Valencia Seydou Keita (Daily Express), Southampton inataka kumsajili beki Neil Taylor kuchukua nafasi ya Luke Shaw (Daily Express), na Bayern Munich imekamilisha usajili wa Ezequiel Garay kutoka Benfica (Clarin), NA HATIMAYE.. beki wa Real Madrid Sergio Ramos amechora tattoo ya Kombe la Champions League kwenye kiwiko cha mguu wa kushoto. Ana tattoo ya Kombe la Dunia kwenye sehemu kama hiyo kwenye mguu wake wa kulia. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho panapo majaaliwa. Adios!
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks