Idara ya Habari ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC) inatarajiwa kupunguza nafasi za kazi 415 kama njia ya kuendelea kupunguza gharama, ametangaza kiongozi wa idara hiyo, James Harding. Hatua hiyo ni sehemu tu ya pauni milioni 800 (Trilioni 2) ya akiba inayotakiwa baada ya kuzuiwa ada ya leseni mwaka 2010...>>>>
Punguzo hilo linatarajiwa kuokoa pauni milioni 48 ifikapo 2017.
Idara ya habari ya BBC kwa sasa imeajiri watu wapatao 8,400, wakiwemo waandishi wa habari 5,000, wakiwa London, Uingereza na nchi nyingine za nje.
Pia ameweka mipango ya kuunda upya utoaji wa habari ili kuifanya BBC kuwa mstari wa mbele kwa kutoa habari kwa kizazi cha kidijitali kwa kutumia teknolojia mpya.
0 comments:
Post a Comment