Special One: ‘Tumeshamaliza kusajili’

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema matumizi ya kikosi chake yamekamilika kufuatia saini ya mlinzi wa kushoto Filipe Luis kutoka Atletico Madrid....>>>

Luis ni mchezaji wa mwisho kusajiliwa The Blues baada viungo Cesc Fabregas na Mario Pasalic na mshambuliaji Diego Costa.
“Tumemaliza kusajili leo”, alisema Mourinho. “Dirisha kuu la usajili litafungwa Agosti 31 na sisi tunalinga leo Julai 19.”
“Klabu yangu imefanya kazi nzuri, sio kwa sababu kwa kile tulichokinunua, ila kwa sababu tumefanya kwenye muda muafaka.”
Chelsea pia ilihusishwa na baadhi ya uhamisho wa gharama, wakiwemo kiungo wa Real Madrid na mshindi wa Kombe la Dunia Sami Khedira na mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao.
Hata hivyo, Mourinho amesisitiza kuwa ameridhishwa na kazi iliyofanywa na klabu yake msimu huu.
“Klabu imefanya kazi nzuri, tulijua tunaowahitaji, tulijua wachezaji na vilabu tukaamua kuwafauta kwenye vilabu vyao mapema”, aliongeza.
“Tumevipata vile tulivyokuwa tukivihitaji. Kikosi hiki nakipenda sana na tuko tayari kuanza msimu”.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks