Maradona aiponda tuzo ya Messi


inaonekana kipigo walichokipata jana kikosi cha Alejandro Sabella kimewachanganya wa Argentina wengi, huku yakiripotiwa baadhi ya matukio ya fujo zilizofanywa na mashabiki wa timu hiyo katika Jiji la Rio De Janeiro baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa na Ujerumani kuibuka mabingwa wapya wa Dunia nchini Brazil....>>>>

Pia inaonekana  ni muda muafaka wa kutupiana lawama, tayari Lionel Messi ameshaanza kuitupia lawama safu ya mashambulizi ya kikosi chao kwa kupoteza nafasi nyingi walizo kuwa wakizipata yani kama ingekuwa ni kisu basi safu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Gonzalo Higuain tungeifananisha na kisu butu kwa kukosa makali.
Wakati hayo yakitokea ndani na njee ya kikosi hicho cha Argentina, Gwiji wa soka wa Argentina mwenye maneno mengi ya utata pindi anapozungumza na vyombo vya habari Diego Maradona, amedai kuwa Lionel Messi hakustahili tuzo aliyoipata jana kama mchezaji bora wa mashindano na kumzidi Neymar, Arjen Robben, Thomas Muller na James Rodriguez waliokuwa wanawania tuzo hiyo.
“Nadhani haikuwa haki kwa Messi kuchukua tuzo ya mchezaji bora, naamini hiyo tuzo aliipata kwa sababu za kibiashara na siyo uwezo au kiwango alichokionyesha katika michuano hii’ alisema maneno hayo wakati  akifanya mahojiano na kituo cha habari cha  “Telesur”.
Lionel Messi 27, alifunga magoli manne na kutoa mchango katika  kikosi chake  kupatikana kwa goli jingine kati ya mechi saba alizocheza na kukisaidia kikosi chake kufika fainali, ambapo katika mchezo huo Ujerumani walipata ushindi wa goli 1-0, Mario Gotze , 22, ndio alikuwa mfungaji wa goli hilo katika dakika za majeruhi kwenye muda wa nyongeza.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks