Nyota wa mpira miguu wa Ujerumani na Arsenal Mesut Ozil anatarajiwa kutoa msaada wa pauni 350,000 (Mil. 875) ya ushindi wa Kombe la Dunia kwa watoto wa Gaza kufuatia ushindi wa nchi yake kwenye mashidano makubwa duniani, kwa mujibu wa Middle East Monitor...>>>
Huku mapigano yakiendelea kwa kasi Mashariki ya Kati baada ya makubaliano ya kuacha mapigano kugonga mwamba, inadaiwa kuwa Ozil yuko tayari bakshishi yake ya pauni 237,000 (Mil. 592.5) aliyoipata kwa kuisaidia Ujerumani kushinda fainali, na pauni 118,000 (Mil. 295) aliyoipata kwenye nusu-fainali, kwa ajili ya eneo hilo lililochukuliwa.
Hata hivyo, Ozil hajathibitisha taarifa za kutoa msaada huo kwa Gaza, kwani kuna madai kuwa pesa hizo anataka kuzitoa msaada Brazil.
Ozil ambaye ana asili ya Uturuki na Muislamu anayefanya ibada na kusoma Quran kabla ya mechi. Alizua utata baada ya kugoma kufunga wakati wa mashindano, ambayo yaliangukia mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo Waislamu hufunga kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Pia imeripotiwa kuwa Ozil alizua tafrani wakati alipogoma kumpa mkono afisa wa Fifa kwa sababu anaiunga mkono Israel.
Siku tisa sasa tangu kuibuke mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas na kuonekana zaidi ya ndege 1000 zikiingia Israel na huku zaidi ya ndege 1,300 zikiushambulia Ukanda wa Gaza.
0 comments:
Post a Comment