2030 watajwa kuwa mwisho wa Ukimwi


Kuna uwezekano wa maambukizi ya Ukimwi kuweza kuzuiwa ifikapo 2030, hii ni kutokana na ripoti ya Shirika la Ukimwi la Umoja wa Mataifa.
Inasemekana kuwa idad ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na vifo kutokana na Ukimwi vimekuwa vikipungua...>>>

Hata hivyo, juhudi za jamii ya kimataifa zinahitajika zaidi kwani “hali ya sasa haiwezi kulitimiza hilo”.
Wafadhili wa Madaktari wasio na Mipaka (Medecins Sans Frontieres) walionya kuwa watu wanaohitaji dawa vya HIV huwa haziwafikii.
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa watu milioni 35 walikuwa wanaishi na HIV duniani kote.
Kulikuwa na kesi mpya milioni 2.1 mwaka 2013, sawa na asilimia 38, ikipungua kutoka milioni 3.4 mwaka 2001.
Vifo vinavyosababishwa na Ukimwi vimepungua mara tano miaka mitatu iliyopita, vikiwa kwenye milioni 1.5 kwa mwaka. Afrika Kusini na Ethiopia pia zimekuwa na mabadiliko.
Sababu zinazochangia picha hiyo ni ongezeka la dawa kwa wagonjwa. Wanaume kutahiriwa na hivyo kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks