Wataalamu wa tiba waelezea faida za ‘ushuzi’


Wanasayansi katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu mbaya kama vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu..>>>

Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani,   Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.
Ndio! athari ni kile ambacho unakidhania: Eti watu wanauchukulia utafiti huu kumaanisha kuwa harufu mbaya inayotokana na mtu kujamba inaweza kuzuia magonjwa fulani mwilini kama vile saratani.
Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.
“Ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kujamba, hutengenezwa mwilini na inaweza kuwa kana tiba kwa magonjwa fulani,” alisema daktari Mark Wood, profesa wa chuo hicho cha Exeter.
Hata hivyo gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo
Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kujamba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu kupatwa na magonjwa kama vile, saratani, kiharusi, mshtuko wa moyo na kuumwa na mifupa.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks