Taarifa mpya juu ya ndege nyingine ya Malaysia iliyoanguka Ukraine.

Wakazi wa eneo ilikoanguka ndege wakiangalia mabaki ya Malaysian Airlines MH17. Picha kwa hisani ya MatevzNovak.
Msiba mwingine mkubwa umeikuta kampuni ya ndege ya Malaysia Airlines baada ya ndege yake moja kuanguka huko Ukraine, katika tukio linaloaminika kuwa imetunguliwa kutokea ardhini...>>>>
Ndege hiyo aina ye Boeing 777 yenye safari namba MH17, iliyokuwa njiani kutoka Amsterdam nchini Uholanzi kwenda Kuala Lumpur nchini Malaysia ilikuwa na watu 295 ndani yake.
Uchunguzi wa awali umeshaanza kubaini endapo ilikuwa ni ajali au ilishambuliwa kwa silaha.
Tayari kumeanza mchezo wa kutupiana lawama kati ya Ukraine na Urusi nchi ambazo zinapakana na zenye uhasama wa kisiasa baina yao.
Kwa mara nyingine kampuni ya Malaysian Airline inajikuta katika mtihani huku ndege yake nyingine ikiwa haijapatikana miezi kadhaa tangu kutoweka ikiwa safarini kwenda China.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks