Diego Costa ndiye mchezaji wa pekee wa Ligi Kuu ya Uingereza kutajwa kuwania tuzo kubwa barani Ulaya....>>>>
Mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid ni mmoja wa wachezaji 10 waliotajwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora Ulaya.
Costa alishinda taji la La Liga Atletico Madrid ila alikosa kunyanyua la Ligi ya Mabingwa baada ya kupoteza kwa mahasimu wao wa mji Real Madrid mjini Lisbon, Ureno.
Kwenye orodha hiyo pia yupo Luis Suarez. Mng’ataji huyo alikuwa na kipindi kizuri msimu uliopita na kuiongoza nchi yake kuwepo kwenye nne bora.
Wengine ni wachezaji watatu, mabingwa wa Kombe la Dunia Ujerumani ambao ni Philipp Lahm, Thomas Muller na Manuel Neuer, wote wakiichezea Bayern Munich.
Naye mshindi wa Ballon D’or Cristiano Ronaldo yupo kwenye orodha pamoja na kutofanya vizuri kwenye Kombe la Dunia.
Lionel Messi, ambaye alishindwa kuiongoza Argentina kuchukua taji la Kombe la Dunia nchini Brazil ametajwa kuwania tuzo hiyo pia.
Wengine ni mfungaji bora wa Kombe la Dunia James Rodriguez, winga wa Uholanzi Arjen Robben na nyota wa Argentina Angel Di Maria.
ORODHA KAMILI
Angel Di María (Argentina, Real Madrid)
James Rodríguez (Colombia, AS Monaco)
Philipp Lahm (Germany, FC Bayern Munich)
Lionel Messi (Argentina, Barcelona)
Thomas Müller (Germany, Bayern Munich)
Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich)
Arjen Robben (Netherlands, Bayern Munich)
Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid)
Luis Suarez (Uruguay, Liverpool FC – now at Barcelona)



0 comments:
Post a Comment