TETESI ZA SOKA ULAYA
*Angel Di Maria kwenda Man U
*Schneiderlin kwenda Arsenal
*Cech kuodoka Darajani
Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez
anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa
pauni milioni 80 kwenda Barcelona katika...>>>>
*Angel Di Maria kwenda Man U
*Schneiderlin kwenda Arsenal
*Cech kuodoka Darajani
Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez
anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa
pauni milioni 80 kwenda Barcelona katika...>>>>
saa 48 zijazo (Daily Mail), dau la Liverpool
la pauni milioni 20 la kumtaka beki Dejan
Lovren limekataliwa na Southampton
(Liverpool Echo), Manchester United
wamepewa Angel Di Maria na Real Madrid
kwa pauni milioni 40. Arsenal, Paris St-
Germain na Juventus pia wanamtaka pia
mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina
(Daily Star), meneja wa Arsenal, Arsene
Wenger ana uhakika wa kuwasajili Alexis
Sanchez na Mathieu Debuchy kwa pauni
milioni 35 (Daily Mirror), washika bunduki
hao pia watatoa dau la pauni milioni 20 kwa
Southampton kumsajili Morgan Schneiderlin,
ambaye anasakwa pia na Napoli (Daily
Express), Bayern Munich huenda wakawazidi
kete Manchester United, Liverpool na
Arsenal kumchukua winga wa Fiorentina,
Juan Cuadrado (Daily Express), Arsenal pia
wametoa dau la pauni milioni 23.8
kumwania kiungo wa Real Madrid, Sami
Khedira na watamtumia rafiki wake wa
karibu Mesut Ozil kumshawishi (Metro), dau
la pauni milioni 32 la Manchester City
kumtaka beki Eliaquim Mangala
limekubaliwa na Porto, lakini bado
wanasubiri kama Chelsea nao pia
watapanda dau (Daily Star), Juventus wako
makini kumsajili beki wa Manchester United
Patrice Evra, ambaye amesaini mkataba
mpya Old Trafford mwezi uliopita (Talksport)
, Barcelona wataajiri mwanasaikolojia wa
kumsaidia Luis Suarez kukabiliana na
'mizimu' atakapokamilisha uhamisho wake
(Sun) QPR wanatarajia kukamilisha usajili
wa Rio Ferdinand wiki ijayo
(GetWestLondon), na kipa wa Chelsea Petr
Cech huenda akaondoka Darajani kabla ya
msimu mpya kuanza, kwa mujibu wa wakala
wake (Talksport). Share tetesi hizi na
wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa. Adios!
0 comments:
Post a Comment