Tetesi za soka katika magazeti ya ulaya

TETESI ZA SOKA ULAYA
*Eto'o, Sanchez kwenda Arsenal?
*Carvalho kwenda Man U
*Adebayor aanza 'kujifua'..>>
Alvaro Negredo anataka kuondoka
Manchester City na huenda akarejea Spain.
City wamesisitiza kuwa mshambuliaji huyo
hauzwi, lakini inafahamika kuwa anataka
kujiunga na Atletico Madrid (Daily Mail),
Manchester United wameambiwa wanaweza
kumsajili kiungo William Carvalho kutoka
Sporting Lisbon, lakini lazima walipe pauni
milioni 37 kutegua kizingiti cha ununuzi
(Daily Express), Everton wamekataa ombi la
Tottenham kumsajili beki John Stones (Sun),
Southampton wamedhamiria kumshikilia
beki wao wa kati Dejan Lovren anayenyatiwa
na Liverpool, Tottenham na Arsenal (Daily
Express), Juventus wanataka kumchukua
beki wa kati wa Man City Matija Nastasic
kwa mkopo ili kuziba pengo la Andrea
Barzagli ambaye amefanyiwa upasuaji
(talksport), mshambuliaji wa zamani wa
Chelsea Samuel Eto'o huenda akasalia EPL-
Arsenal na Everton wanafikiria kumchukua
(Talksport), beki wa Atletico Madrid Filipe
Luis atalazimika kulazimisha uhamisho
wake kwenda Chelsea baada ya
mazungumzo kati ya timu hizo mbili
kudorora (Daily Star), Arsenal na Liverpool
watagombea kusaka saini ya nyota wa Chile
na Barcelona Alexis Sanchez ambaye
huenda akagharimu pauni milioni 30 (Daily
Mail), Harry Redknapp amekuwa akizozana
na wakuu wa QPR kuhusiana na kutaka
kumsajili Rio Ferdinand aliyekuwa Man
United (Daily Mirror), Galatasaray wametoa
mkataba wa pauni milioni 3 kwa msimu
kumshawishi Samuel Eto'o (Le Figaro),
Diego Maradona atafanya mazungumzo
kuhusiana na kupewa kazi ya kuifundisha
timu ya taifa ya Venezuela (Guardian), na
hatimaye mshambuliaji wa Tottenham
Emmanuel Adebayor tayari ameanza
mazoezi kujiandaa na msimu mpya- na
zoezi zaidi analofanya ni mitindo mipya ya
kushangilia goli. Tafadhali share tetesi hizi-
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks