Uruguay yenye umri wa miaka 27.
Suarez mwenye mkataba wa miaka minne na
timu yake ya Liverpool bado anaendelea
kutumikia adhabu yake yakutojihusisha na
maswala yoyote ya soka kwa miezi minne
mara baada ya kumng’ata beki wa Italia
Georgio Chiellini katika mechi ya Kombe la
Dunia nchini Brazil.
Liverpool wapo tayari kumuuza Suarez kwa
ada ya pauni milioni 80,inaonekana thamani
yake imepanda haswa ukizingatia mwaka
2011 alisajiliwa kwa ada ya pauni milioni
22.7 kutoka Ajax.
Hatahivyo, Barcelona ipo tayari kutoa ada ya
uhamisho wa inayokaribia pauni milioni 60.
Pia katika uhamisho huo Barcelona inatarajia
kumjumuisha winga wao Alexis Sanchez kama
sehemu ya makubaliano yao katika
kubadilishana wachezaji.
Bado haijawekwa wazi kama Alexis Sanchez
atakubalii kujumuishwa katika uhumisho huo
nakuja kuichezea Liverpool,ingawaje timu hiyo
kutoka jimbo la Catalunya ipo tayari kumuuza
mchezaji huyo kwenda Anfield.
Inaonekana Barcelona hawapo tayari kutoa
pauni milioni 80 haswa kutokana na Suarez
kupatikana na hatia ya kumng’ata beki wa
Italia Georgio Chiellini kwa sababu wanahisi
thamani yake itakua imeshuka, lakini tusubiri
tuone yatakayojiri katika mkutano huo.

0 comments:
Post a Comment