Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assa
Mwambene. Mwambene amesema mpaka sasa
chanzo cha kifo cha balozi huyo
Msemaji wa serikali hapa nchini Assa
Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha
Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail
Nwairat kwa kujipiga risasi mwenyewe majira
ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za
ubalozi huo.
Mwambene alisema kuwa mpaka sasa
haijafahamika kifo cha balozi huyo
kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu
katika ubalozi huo wamesema kuwa walisikia
mlio wa risasi chumbani kwake, na
walipojaribu kufungua mlango ulikuwa
umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja
mlango huo na kufanikiwa kumkuta balozi
yupo katika hali ya mbaya.
Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami
iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa
madaktari walithibitisha kuwa amefarika
dunia.
Serikali imesikitishwa na kifo hicho na
wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha
mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao
kwa ajili ya mazishi.

0 comments:
Post a Comment