Miroslav Klose aungana na Philipp Lahm Ujerumani


Miroslav Klose wa Ujerumani amestaafu soka la kimataifa huku akiwa na rekodi kama mfungaji anayeongoza kwa kufunga magoli 16 kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.
Miroslav Klose wa Ujerumani amestaafu soka la kimataifa huku akiwa na rekodi kama mfungaji anayeongoza kwa kufunga magoli 16 kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.
Mfungaji anayeoongoza kwa vipindi vyote Ujerumani Miroslav Klose ametangaza kustaafu soka la kimataifa...>>>

Mshambuliaji huyo wa Lazio, 36 aliisaidia nchi yake kushinda Kombe la Dunia katika msimu wa jua, na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji kwenye historia ya mashindano hayo.
Klose ana jumla ya magoli 71 katika mechi 137, alikuwa mchezaji wa tatu kufunga kwenye fainali za Kombe la Dunia la nne.
Aliyekuwa nahodha wa Ujerumani Philipp Lahm alitangaza kustaafu soka la kimataifa mwezi Julai.
Aliyekuwa nahodha wa Ujerumani Philipp Lahm alitangaza kustaafu soka la kimataifa mwezi Julai.
“Nina furaha na ninajivunia kutoa mchango kwenye mafanikio makubwa ya soka la Ujerumani,” alisema Klose.
Klose, mzaliwa wa Poland alifunga magoli mawili kwenye mashindano nchini Brazil na kumpiku Mbrazil Ronaldo kwenye ushindani na kuweka rekodi ya magoli 16, alisema muda ulikuwa sawa kumaliza maisha yake ya soka ya miaka 13 na timu ya Ujerumani.
Klose ni mchezaji wa pili wa Ujerumani kustaafu baada ya nahodha Philipp Lahm aliyefanya hivyo mwezi uliopita.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks