Liverpool wanafikiria kumnyakua mkongwe mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto’o huku Brendan Rodgers akitaka kuongeza nguvu sehemu ya ushambuliaji kabla ya kipindi cha kusajili kufikia tamati.
Eto’o 33, ni mchezaji huru ambaye ameachwa na Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita na ameshafanya mazungumzo na Ajax ili kwenda Amsterdam...>>>
Liverpool hawajatangaza dau mpaka sasa kwa mfungaji huyo wa zamani wa Real Madrid, Barcelona, Inter Milan, na washataja baadhi ya majina ila Eto’o anaonekana kuwa mlengwa mkubwa.
Inaaminika kuwa mshambuliaji huyo alijiingizia pauni milioni 7 kwenye mkataba wake wa mwaka mmoja Stamford Bridge, ukishuka kutoka pauni milioni 13 kwenye mkataba wake na Anzhi Makhachkala, ila mahitaji yake ya mshahara hayaonekani kuisumbua Liverpool kwa mchezaji ambaye ni huru.
Rodgers bado ana malengo ya kuongeza mshambuliaji kwenye kikosi chake kabla ya Septemba 1, ameshamuuza Luis Suarez kwenda Barcelona kwa pauni milioni 75 na kushinda kumnyakuwa Loic Remy kwa pauni milioni 8 kutoka Queens Park Rangers.
0 comments:
Post a Comment